Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza
wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano yautawala
wake
Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
1.Profesa Jumanne Maghembe -Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili
na Utalii.
2.Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na
Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).
3.Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na
Umwagiliaji.
4.Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa
Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi.(Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)
5.Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi
6.Prof.Makame Mbarawa –Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na
Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano
Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za
Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015

0 comments:
Post a Comment